TAARIFA YA USHIRIKI WA NANE NANE

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
MVIWATA – KAGERA
S.L.P 80
MULEBA- KAGERA- TANZANIA
Simu: +255 788
685 818/ +255 752 751 074
TAARIFA YA USHIRIKI WA
NANENANE 2016

Banda la MVIWATA Kagera katika maonyesho ya nanenane 2016 la kuonyesha
kauli mbiu ya MVIWATA
1.Utangulizi
MVIWATA Kagera imeshiriki
maonyesho ya nanenane mkoani kagera mwaka 2016 kwa kuwezeshwa na MVIWATA Taifa.
Katika maonyesho walishirikishwa
wakulima watano walioweza kuonyesha :-
Ø Ijue MVIWATA
Ø Ufugaji wa nyuki
Ø Ufugaji wa samaki
Ø Ufugaji wa kwale
Ø Shughuri zilizofanyika katika mradi wa PETS.
Jumla ya viongozi na
wananchi wapatao 160 walifika katika banda la MVIWATA Kagera kuhoji
na kupata ufahamu wa shughuri za MVIWATA kwa ujumla.
2.Shughuri Kuu Za Mviwata
Kupitia ushiriki huu,Tuliandaa vitini ,vitabu na
vipeperushi na picha vinavyoelezea
shughuli kuu za MVIWATA na kuwapatia washiriki ili pamoja na maelezo
viwasaidia kujisomea kwa uelewa zaidi:-
·
Kitini kinachoelezea shughuli za MVIWATA(fungua
hapa chini)

·
Vitabu mbalimbali
Mkuu wa mkoa Kagera Ndg Luteni general Samwel Kijuu na
viongozi wa seikali wakipata maelezo ya shughuli kuu zinazofanywa na MVIWATA
toka kwa promota Jovita Juston wa kikundi cha Tunaweza akiba na Mikopo Gwanseli
Vitini
na vitabu mbalimbali katika kuelezea shughuli za MVIWATA
3.Ufugaji Wa
Nyuki:-
Kwakuwa
vikundi vinajiusisha na ujasiliamali kikundi cha chapakazi kimeonyesha kwa
vitendo ufugaji wa nyuki kwa kuweka mizinga ya kisasa, mavazi ya kuzuia usalama, Asali na vifaa vya kuvunia kama inavyoonekana
hapa kweye picha- 

Mkuu wa mkoa Kagera Ndg Luteni general Samweli Kijuu na
viongozi wa serikali wakipata maelezo ya ufugaji wa nyuki toka mkulima Peles
Baguma wa kikundi cha chapakazi Mubunda

Mkuu wa mkoa Kagera Ndg Luteni general Samweli Kijuu na
viongozi wa serikali wakipata maelezo ya kazi za vikundi yva wakulima
4.Ufugaji wa samaki:-
Kwakuwa
vikundi vinajiusisha na ujasiliamali kikundi cha Busara kimeonyesha kwa vitendo ufugaji wa samaki kwa kuweka vifaranga wa samaki, vifaa vya
kuvunia na chakula kama inavyoonekana
hapa kwenye picha-
Mkuu
wa mkoa Kagera Ndg Luteni general
Samweli Kijuu na viongozi wa serikali wakipata maelezo yza ufugaji wa samaki
toka mkulima Kajubu wa kikundi cha Busara gwanseli
5.Ufugaji wa Kwale
Kwa kuwa
vikundi vinajiusisha na ujasiliamali kikundi cha Kaweso kimeonyesha kwa vitendo ufugaji wa kwale kwa kuweka vifaranga na mashine ya kutotoa na
kwale waliofugwa kama inavyoonekana hapa
kwenye picha-

Mkuu wa mkoa Kagera Ndg Luteni general Samweli Kijuu na
viongozi wa serikali wakipata maelezo ya ufugaji wa kwale toka mkulima Kajubu
wa kikundi cha Busara gwanseli

Picha ya namna ya utotoaji vifaranga
vya kwale kwa kutumia incubator
6.Shughuri zilizofanyika katika mradi wa PETS.
Kupitia ushiriki huu,Tuliandaa vitini ,vitabu na
vipeperushi na picha vinavyoelezea
shughuli za PETS na kuwapatia washiriki ili pamoja na maelezo viwasaidia kujisomea kwa
uelewa zaidi:-
Ø
Kitini kinachoelezea shughuli za PETS(fungua hapa)

Ø
Picha
za matukio ya PETS
Mkuu
wa mkoa Kagera Ndg Luteni Samweli Kijuu na
viongozi wa serikali wakipata maelezo ya shughuli za PETS kutoka kwa mtendaji
wa pets Mr Projestus Ishekanyoro
Picha
za miradi scheme za umwagiliaji na masoko yaliokwama tangu 2006
Ø Picha za majukwaa na watunga sera katika kupokea taarifa za
utekekelezaji shughuri za PETS
Picha
ya miche bora ya kahawa inayozalishwa na wakulima
MVIWATA Kagera tunatoa shukrani kubwa kwa
menejimenti ya MVIWATA kusaidia kuwezesha kifedha ushiriki wa
Nanenane Bukoba 2016, kwani imesaidia kupanua wigo wa kufahamika hasa kwa
vingozi wapya baada ya uteuzi wa Mhe Raisi.
Wako,
Projestus Ishekanyoro
K.n.y kamati ya uongozi MVIWATA Kagera
Comments
Post a Comment