REPORTS OF MVIWATA
Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
(Network of
Farmers’ Groups in Tanzania)
P. O. Box 80 Muleba - Kagera
Taarifa ya Utekelezaji Shughuli za
MVIWATA Kagera kwa kipindi cha Miezi Mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2015
1. Utangulizi
Hii ni taarifa ya shughuli za MVIWATA
Kagera za miezi mitatu, Januari hadi Machi 2015. Taarifa hii inawasilishwa kwa
njia ya jedwali lililopo hapa chini. Kwa ujumla shughuli hizi zinafuata Mpango
Mkakati wa MVIWATA wa 2010 – 2014 na pia Mpango Kazi wa MVIWATA Kagera Januari
– Disemba 2015.
Mkakati 1: Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kuwawezesha
kujipanga na kujitetea.
|
Shughuli iliyopangwa
|
Hali ya Utekelezaji
|
Matokeo
|
|
1.
Kuimarisha mitandao ya msingi na
vikundi ili kuweza kutoa huduma kwa wanachama.
|
Katika kipindi cha Jananuari-March 2015, shughuli kuu
iliyofanyika ni kuhamasisha uanzishwaji vikundi, mikutano mikuu ya mitandao ya
misingi na vikundi na kuimalisha mitando iliyopo.
Kikundi
cha AMANI Muhutwe
|
Mitandao ya msingi
mitano imefikiwa na nakufikia
wanachama 106 (ME 61 KE 45) kati yao wanachama wapya ni 22 (ME 14 KE
8) kama ifuatavyo:-Buganguzi (ME 7), Gwanseli 42, KE 16 ME 26 Muhutwe 11 ME 3
KE 8, Kashasha 28 KE 11 ME 17 na Mubunda 18 KE 10 ME 8.
|
|
2.
Kuada na kutoa mafunzo kwa viongozi
wa mitandao na vikundi ngazi ya kati.
|
Hajafanyika
|
|
|
3.
Kuandaa taarifa za wanachama, ulipaji
wa ada za vikundi na kubaini wanachama wapya.
|
Kufikia tarehe 30/3/2015 tumefikia wanachama 925 wenye
kadi za MVIWATA na wanachama wanufaikaji 2323 jumla 3248, vikundi 127 na
mitandao 36.
|
Kupata wanachama wapya – vikundi 7, wanachama 22 na vikundi 7 kulipia ada ya mwaka 2015.
(orodha ya vikundi
vipya na majina ya wanachama na vikundi vilivyo lipa ada imeambatanishw
|
Matarajio:
Kuhakikisha kuwepo Vikundi na Mitandao
Imara ya Wakulima ambayo Inawajibika katika kutekeleza majukumu yao
Mkakati
2: Ushawishi na Utetezi: kuwezesha
wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kushawishi na kutetea maslahi yao na kuongeza
ushiriki na ushikishwaji wao katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa
katika ngazi ya msingi, kitaifa na kimataifa.
Tarajio 1: Kuwepo mkakati wa Ushawishi na Utetezi wa MVIWATA Kagera.
|
1.
Kufanya tafiti mbalimbali juu ya
masuala yanayogusa masilahi ya mkulima mdogo na kutoa matokeo.
|
·
Kukutana na watafiti wa mazao ya
kilimo ili kujua chanzo cha ugonjwa wa Mnyauko wa migomba na kuutafutia
ufumbuzi – ilionekana ni ugonjwa wa bacteria
isiyotibika inayoenea kwa njia ya hewa.
·
Kufanyika kwa utafiti wa kushuka kwa
zao la kahawa uliofanywa na watafiti kutoka SUA Morogoro Dr. Fatihiya Masawe
na Ndg, Rogers Andrew kwa kushirikiana na MVIWATA Taifa.
|
Sheria ya ukandishaji wa mashamba
imetumika kwa kila mkulima kukata mgomba ulioathirika na kwa sasa ungonjwa wa
myauko unaendelea kupungua.
|
Tarajio
2: MVIWATA inatambulika vizuri kama
taasisi yenye uwezo na nguvu kufanya ushawishi na utetezi kwa masilahi ya
wakulima wadogo.
|
1.
Kuandaa na kuwezesha mafunzo ya
kujenga uelewa wa wakulima juu masuala yanayoathiri ustawi wa wakulima wadogo.
|
Kamati ya PETS ya wilaya na Madiwani wa kata tano
kushiriki mdahalo wa wa kitaifa juu ya Azimio la Umoja wa Afrika kuhusu
kuwekezaji wa kilimo na usalama wa chakula lililoyofanyika Dar es salaam
tarehe 28/2/2015 kwa ushirikiano wa ESAFF
Anayechangia ni Mhe. Diwani Kata
Mubunda Ndg. Kalinjuma. A. Kamili
|
Kamati ya pets 15 Me8 Ke7 na madiwani 5 (ME) kutoka Wilaya
Muleba, kujua azimio la Maputo/Malabo juu ya utekelezaji wa bajeti ya kilimo
kufikia 10%.
Ndg. Projestus
Ishekanyoro akiwasilisha mada ya fursa na vikwazo katika utekelezaji wa PETS
Muleba
|
|
2.
Kuwezesha mafunzo ya kujengea uwezo
viongozi wa vikundi na mitandao juu ya dhana ya ushawishi na utetezi ili
kujenga hadhi ya taasisi ya MVIWATA Kagera.
|
Haijafanyika
|
|
Tarajio 3: Kuimarisha mawasiliano na upashanaji habari ndani na nje ya
MVIWATA Kagera.
|
1.
Kusambaza majalida na machapisho
mbalimbali ya MVIWATA hasa gazeti la pambazuko, taarifa za kila mwezi
yanayohusu shughuli za shirika.
|
Mauzo ya jarida la pambazuko toleo
no.042 hamsini yameuzwa.
|
Mauzo majarida Tshs 50,000/=
imepokelewa
|
|
Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za
MVIWATA Kagera 2014 imetolewa.
|
Tarifa imepokelewa na MVIWATA Taifa,
Halmashauri za Wilaya Muleba na Misenyi, Mkuu wa Wilaya Muleba na Afisa
Tawala wa Mkoa.
|
Mkakati
3: Kuimarisha uwezo wa kiuchumi kwa
lengo la kuwezesha wakulima wadogo kuwa
na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuwaunganisha na masoko
kwa kuwapatioa elimu ya ujasiriamali ili kupunguza umasikini.
Tarajio:1 Kuboresha mifumo ya masoko kwa ajili ya wakulima wadogo.
|
Shughuli iliyopangwa
|
Shughuli zilizotekelezwa
|
Matokeo
|
|
Kufanyika ushawishi juu ya masoko ya zao
la Ndizi na Kahawa.
|
Kupitia vikao vya watoa maamuzi kuelezea tatizo
ukosefu wa masoko ya wazalishajiwadogo.
Kikao cha baraza
la Madiwani Muleba
|
Ujenzi wa soko la Ndizi Muleba mjini unaendelea.
Serikali imeunda timu ya utafiti wa
soko la kahawa na kutoa vibali kwa wanunuzi binafsi.
|
Tarajio
2: Uwezo wa wakulima umeongezeka katika
huduma za kuweka nakukopa kupitia vyombo vyakuweka na kukopa.
|
Kuwezesha mafunzo juu ya faida za
kuweka na kukopa na mbinu za uanzishwaji na uimalishaji vyombo vya kuweka na
kukopa.
|
Mafunzo ya waweka hazina wa SACCOS
yaliyoandaliwa Halmashauri ya wilaya Muleba tarehe 10 – 14/02/2015, Waweka
Hazina wa SACCOS za wanachama MVIWATA tano walishiriki kwa siku nne.
Mafunzo ya Dhana ya VICOBA
yaliyofanyika Mwanza tarehe 23-27/03/2015, viongozi wa SACCOS za MVIWATA
Watatu wameshiriki.
Bi. Jovitha
kushoto na washiriki wengine katika mafunzo ya Waweka Hazina wa SACCOS
|
Muleba Farmers Network SACCOS imepata cheti safi
cha ukaguzi.
|
Mkakati
4: Masuala mtambuka kwa kujenga uelewa
wa wakulima wadogo juu ya athari za UKIMWI, jinsia na mabadiliko ya tabia Nchi,
na mwisho ujenzi wa kitaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika la MVIWATA
Kagera.
Tarajio
1: Masuala ya VVU/UKIMWI yameingizwa
katika mipango ya MVIWATA na kuna uelewa
wa kutosha kwa kwa wanachama, viongozi na watumishi.
|
1. Kutoa mafunzo na uhamasishaji juu
wa wakulima kujikinga na VVU na kuwauganisha wakulima taasisi wa zinazotoa
huduma ya upimaji.
|
Haikufanyika
|
|
Tarajio2: Masuala kuhifadhi misitu ili kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi.
|
1.Kubaini na kutenga hifadhi ya mistu jamii katika maeneo ya
serikali za vijiji.
|
Kusajili mstu jamii Nyakabango na
kuunda kamati ya hifadhi mistu na kupisha sheria ndogo ndogo za vijiji.
|
Usajili na sheria ya kuhifadhi umepatikana
kutoka kwa Halmashauri ya wilaya Muleba.
|
Mkakati 5:ujenzi wa shirika Kitaasisi:
|
1. Kufanya vikao vya kikatiba kwa kamati
ya uongozi,kamati za PETS na kikao cha mapromota.
|
Kikao kimoja cha kamati ya Uongozi
kimefanyika tarehe 7/1/2015.
|
Ø Kupitisha mpango kazi na bajeti wa mwaka 2015
Ø
Kuandaa mpango kazi na bajeti wa miezi mitatu
Ø
Kukagua na kuona mapato na matumizi
ya mwaka 2014
|
|
|
Kikao cha kamati ya PETS kimefanyika
|
Ø
Kukusanya taarifa za PETS kutoka kata
tano.
Ø
Kuandaa watakao shiriki kongamano la PETS
Dar es saalam.
Ø
Kuandaa mpango kazi na bajeti wa PETS Jan –March 2015
|
|
2.Usimamizi na uendeshaji wa ofisi
|
·
Kupokea ada za vikundi Tshs 240,000/=
·
Kupokea viingilio vya wanachama
wapyaTshs 40,000/=
·
Ulipaji wa gharama za uendeshaji wa ofisi
|
·
Malipo ya 30% za ada Tshs 24,000/=
·
Computer ANTIVIRUS DESK TOP and
LAPTOP Tshs 40,000/=
·
Ulipaji wa pango la ofisi Jan- march
2015 Tshs 180,000/=
·
Ununuzi wa kadi za wanachama Tshs 20,000/=
|
Comments
Post a Comment