REPORT FOR SIXTH ANNUAL MEETING -IN SWAHILI
MKUTANO MKUU NGAZI YA KATI KAGERA
UKUMBI WA CALFONIA MULEBA MJINI TAREHE
26/06/2014
MADA: PETS, UMILIKI WA ARDHI, 10% YA BAJETI YA KILIMO NA
MASOKO
Baadhi ya Washiriki kushoto waliokaa
Ndg. P Ishekanyoro(Mjumbe Bodi ya Taifa), J. Rwakyendera (M/Mwenyekiti , P. Ngaiza
Mwenyekiti, Mhe.Lembris Kipuyo Mkuu wa Wilaya Muleba, Mr. T. Mbowe na Mr. T.
Mtandu Vi Agroforestry
TAARIFA YA MAENDELEO NGAZI YA KATI
KAGERA
Taarifa ilizingatia idadi ya vikundi
234 vyenye wanachama 3123, utume wa shirika, dira ya shirika, shughuli kuu
zilizofanyika, mafanikio, changamoto, Mpango Mkakati wa MVIWATA Kagera, Mapato
na matumizi Januari hadi Mei 2014 na ombi kwa mgeni rasmi iliyowasilishwa na
Mwenyekiti MVIWATA Kagera Ndg. Ponsian Ngaiza. Mkutano huu walishiriki wanachama
50 ME 33, KE 17, Wataalamu wa kilimo na misitu pamoja na wageni toka Vi
Agroforestry
UFUNGUZI
WA MKUTANO MKUU
Mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Wilaya Ndg.
Lembris Kipuyo, kabla ya ufunguzi wa mkutano, alishukuru uogonzi na wanachama
wa MVIWATA Kagera kumualika katika mkutano huu muhimu.
Katika hotuba alipongeza jitihada
zinazofanywa na MVIWATA TAIFA kuwaunganisha wakulima kuwa na sauti moja,pia
Mgeni rasmi kuwaekeza wakulima kuwa na
mipango mikubwa endelevu ikiwemo miundo mbinu,masoko na viwanda.
Mgeni rasmi alitoa agizo kwa wataalamu
waliomo wilayani kushirikiana na
wakulima kutatua changamoto zinazowakabili wakulima katika shughuli za
uzalishaji ikiwemo suala la PETS, Masoko, Magonjwa ya mimea kama Myauko,
umiliki wa aridhi na hifadhi misitu jamii na kuhaidi ushirikiano mkubwa pale
atakapohitajika pamija na kuweka mawasiliano yake wazi. Baada ya hapo mkutano
umefunguliwa saa 4:30 asubuhi.
MADA KUU ZA MKUTANO
1. Wakulima juu ya Mapato na Matumizi ya
Pesa za Umma (PETS)
Trainer of Trainers (TOT) Ndg.
Projestus Ishekanyoro aliwashirikisha washiriki wa mkutano maana ya PETS, faida
za PETS, haki za mkulima kushiriki PETS na changamoto wanazokumbana nazo katika
utekelezaji wa PETS.
Ndg. Projestus Ishekanyoro akiwasilisha Mada ya PETS
katika Mkutano Mkuu MVIWATA Kagera
2. Ushiriki
wa Mkulima katika Bajeti ya Serikali
Mada hii iliwasilishwa na Ndg. D.W.
Lwekamwa (PAFOI) ambapo aliwashirikisha
wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kuwafafanulia kuwa zamani Mipango ilikuwa ikipangwa
kuanzia ngazi za juu (TOP BOTTOM APPROACH ambayo miradi mbalimbali haikuwa
endelevu kwa kuwa haikuwa hitaji la wakulima. Kwa sasa bajeti ni shirikishi
(BOTTOM UP APPROACH).
3. Wajibu
wa Kuhifadhi Misitu Jamii
Mada
husika iliwasilishwa na Ndg. Lugano Ambakisye (FO) ambapo alitoa changamoto za
kimazingira zinazowakabili wakulima kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hali
inayochangiwa na uhifadhi duni wa misitu. Aliwasihi wakulima watenge maeneo ya
uhifadhi wa misitu jamii na kuzifuata sheria zilizopo ili kwa pamoja kupambana
na mabadiliko ya tabia nchi kwa uzalishaji endelevu.
4. Madhara
ya na jinsi ya kupambana na Ugonjwa wa Myauko wa Migomba
Ndg. Daudi Kingu (Afisa Kilimo)
alielezea madhara ya Mnyauko wa Migomba, hatua zilizochukuliwa mpaka sasa na
kuwaomba wakulima kuchukua hatua za awali ambazo ni kuondoa maua dume, kukata
na kuchimbia mgomba ulioathirika na tayari sheria ipo kwa watakaopuuzia
kuchukua hatua.
Comments
Post a Comment