Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania MVIWATA – KAGERA S.L.P 80 MULEBA- KAGERA- TANZANIA E-mail: mviwata.kagera@yahoo.com/ Website: www.mviwata-kagera.blogspot..com Simu: +255 788 685 818/ +255 752 751 MATOKEO YA UBIA WA MVIWATA –Kagera NA ANSAF . 1.Utangulizi. MVIWATA(Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania) ni chombo cha kuwaunganisha wakulima wadogo ili kuwawezesha kuwa na sauti ya pamoja katika kufikia fursa za kijamii,kiuchumi na kisiasa kwa njia ya ushawishi na utetezi.Mviwata Kagera ni tawi la Mviwata Taifa.Mviwata Kagera inafanya kazi katika mkoa kagera,mpaka sasa tumeweza kufikia wilaya ya tano.( Muleba, Bukoba, Misenyi, Ngara na Karagwe) na ofisi yake ipo wilaya Muleba Mjini. MVIWATA- Kagera iliomba ubia na ANSAF katika kuhakikisha maendeleo ya sekita ya kilimo na kuwajengea uwezo wakulima wadogo kudai haki zao. ANSAF kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa kuhakikisha uwaj...